KIPINDI CHA KWANZA.
Mwalimu: OCTAVIAN KIYVIRO
SOMO: KUTAMBUA KUSUDI
LA MUNGU/ KUJUA KUSUDI LA MUNGU.
Matendo 17:11-12”Watu
hawa walikuwa waungwana kuliko wale wathesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno
kwa uelekevu wa Moyo,wakayachunguza maandiko kila siku,waone kwamba mambo hayo
ndivyo yalivyo.Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa kiyunani
wenye cheo, na wanaume si wachache”.
- Tuchunguze maandiko ili tuweze kujua Mungu anazungumza nini kuhusu, Urafiki,Uchumba na ndoa.
Mithali
25:2”Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo,Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza
jambo”
- Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo ili sisi tuchunguze.
- Inatupasa Kutambua na kujua kusudi la Mungu.
- Kuna kusudi au sababu ya Mungu katika sehemu uliyozaliwa.
Mathayo 1:18-21”Kuzaliwa kwake Yesu
Kristo kulikua hivi.Mariam mama yake alipokua ameposwa na Yusufu,kabla
hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho mtakatifu.Naye Yusufu
mumewe kwa vile alikua mtu wa haki,asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa
siri.Basi alipokuwa akifikiri hayo,tazama malaika wa Bwana alimtokea katika
ndoto, akisema, Yusufu mwana wa daudi usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana
mimba yake ni kwa uwezo wa Roho mtakatifu.Naye atamzaa mwan, nawe utamwita jina lake Yesu,maana, yeye ndie
atakae waokoa watu wake na dhambi zao”.
- Kuna sababu za Mungu kukufanya uwepo duniani.
- Inatupasa kutafuta kusudi la Mungu.
Yeremia 1:4-5”Neno la Bwana
lilinijia, kusema kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua,na kabla hujatoka
tumboni nalikutakasa,nimekuweka kuwa nabii wa mataifa”
- Tutambue Kusudi la Mungu kwanza kwenye Maisha yetu.
Hekima ya sulemani 7:3-6
- Yosefu alitambua kusudi la Mungu
- Tutambue Muunganiko wa neno la Mungu na mahusiano.
Waamuzi
13:1-5”Malaika wa Bwana akamtokea Yule mwanamke akamwambia tazama wewe sasa
u tasa huzai,lakini utachukua mimba, nawe utazaa mtoto mwanamume.Basi sasa
jihadhari ‘nakuomba usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi,
kwani tazama utachukua mimba nawe utamzaa mtoto mwanamume, na wembe usipite juu
ya kichwa chake,maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni naye
ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya wafilisti”
Mwanzo 1:26-28”Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.Mungu akawabariki , Mungu akawaambia, zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kutiisha, mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani,na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”
Mwanzo 5:2”Mwanamume na mwanamke aliwaumba ,akawabariki akawaita
jina lao Adam,siku ile walipoumbwa”
“ Aperson is Soul, Spirit and Body”(Nafsi , Roho na Mwili)
Mwanzo 2:4b-7
Mwanzo 2: 19,20.
=======================================================================
KIPINDI CHA PILI.
Mwalimu: ROBART MITTI
SOMO:KUJUA KUSUDI LA
MUNGU
Matendo 17:10
Waamuzi 13:4”Basi
sasa jihadhari, nakuomba usinywe divai wala kileo, wala usile kitu
kilichonajisi”
Kusudi la Mungu kwako ni nini?
Mathayo 1:18-21
Zaburi 8:3-5 na 6-9
- Wewe umefanyika kuwa mwana wa mfalme.
- Tusiwatazame Waberoya wakabaki kuwa Waberoya,tuyachunguze maandiko ili tujue kusudi la Mungu katika maisha yetu.
- Tunaitwa kuishi kama mfalme.
Yoshua Bin Sira 23:16-17”Hapo
mtakapo livunja agano la Bwana, Mungu wenu alilowaamuru, na kwenda kuitumikia
miungu mingine na kujiinamisha mbele yao, ndipo hasira ya Bwana itakopowaka juu
yenu, nanyi mtaangamia upesi katika nchi hii njema aliyowapa”
- Tusikubali kutikiswa (Unshakable)
- Si rahisi kutimiza mapenzi ya Mungu Kama hatutotimiza kusudi la Mungu katika maisha yetu.
2 Mambo ya Nyakati 7:12-14”Bwana akamtokea sulemani usiku,
akamwambia nimesikia uliyoyaomba,na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya
dhabihu.Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi,au
nikiwapelekea watu wangu tauni.ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu
watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso,na kuziacha njia zao mbaya, basi
nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao,na kuiponya nchi yao”
- Tambua nafasi yako kama kijana wa kike na wa kiume utimize kusudi la Mungu kwako.
KAZI TATU KUU ZA ROHO MTAKATIFU
- Kutusaidia kuomba jinsi Mungu anavyotaka tuombe.
- Kudhihirisha Matendo makuu ya Mungu.
- Roho mtakatifu kudhihirishwa ulimwenguni kwa habari ya dhambi.
Zaburi
32:8”Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea,Nitakushauri jicho
langu likikutazama”.
Isaya
30:21” Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako,likisema, njia
hii,ifuateni mgeukapo kwenda mkono wa kulia na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto”
Mhubiri
4:8…
3
Yohana 1:11-13.