JIFUNZE BIBLIA TAKATIFU
IMANI
Basi imani, chanzo chake ni
kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. - [Warumi 10:17]
Mtumaini Bwana kwa moyo wako
wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye,
Naye atayanyosha mapito yako. - [Mithali
3:5,6]
Yesu akamwambia, Ukiweza!
Yote yawezekana kwake aaminiye. - [Marko
9:23]
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani
ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. - [2 Wakorintho 5:17]
kwa kuwa hakuna neno
lisilowezekana kwa Mungu. - [Luka 1:37]
Ndipo alipowagusa macho,
akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate. - [Mathayo 9:29b]
Basi imani ni kuwa na hakika
ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. - [Waebrania 11:1]
Lakini mtu wa kwenu
akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala
hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana
mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa
huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. Mtu
wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote. - [Yakobo 1:5-8]
Lakini pasipo imani
haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba
yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. - [Waebrania 11:6]
Maana kama vile mwili pasipo
roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa. - [Yakobo
2:26]
Na kila tendo lisilotoka
katika imani ni dhambi. - [Warumi 14:23b]
Lakini mwenye haki wangu
ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. - [Waebrania
10:38]
Tazama, ataniua; sina
tumaini; ila hata hivyonitaithibitisha njia yangu mbele yake. -
[Ayubu 13:15a]
Nguvu zenu zitakuwa katika
kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. - [Isaya 30:15b]
Kama sisi hatuamini, yeye
hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. - [2 Timotheo 2:13]
Kwa maana kila kitu
kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako
ulimwengu, hiyo imani yetu. - [1 Yohana 5:4]
Zaidi ya yote mkiitwaa ngao
ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule
mwovu. - [Waefeso 6:16]
Yesu akawaambia, Kwa sababu
ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha
punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka;
wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. - [Mathayo 17:20]
tukimtazama Yesu, mwenye
kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa
mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume
wa kiti cha enzi cha Mungu. - [Waebrania 12:2]
Basi tukiisha kuhesabiwa haki
itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu
Kristo, - [Warumi 5:1]
Yesu akajibu, akamwambia,
Mwaminini Mungu. - [Marko 11:22]
Mnafurahi sana wakati huo,
ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu
ya namna mbalimbali; ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani
kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa
kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. Naye
mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na
kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, katika kuupokea mwisho wa
imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. - [1 Petro 1:6-9]
UPENDO
Akasema, Uso wangu utakwenda
pamoja nawe, nami nitakupa raha. [Kutoka 33:14]
Hata walipokuwa wakishuka
mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye
akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu. [1
Samweli 9:27]
Naye akawaambia Yuda, Na
tuijenge miji hii, na kuizungushia maboma, na minara, na malango, na makomeo;
nchi bado ikalipo mbele yetu, kwa kuwa tumemtafuta Bwana, Mungu wetu; naam,
tumemtafuta, naye amemstarehesha pande zote. Basi wakajenga, wakafanikiwa. [2
Mambo ya Nyakati 14:7B]
Mwe na hofu wala msitende
dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia. [Zaburi 4:4]
Umngoje Bwana, uwe hodari,
Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana. [Zaburi 27:14]
Ukae kimya mbele za Bwana,
Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala
mtu afanyaye hila. [Zaburi 37:7]
Nalimngoja Bwana kwa saburi,
Akaniinamia akakisikia kilio changu. [Zaburi 40:1]
Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni
Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi. [Zaburi 46:10A]
Umtwike Bwana mzigo wako naye
atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele. [Zaburi 55:22]
Enyi watu, mtumainini
sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. [Zaburi
62:8]
Utamlinda yeye ambaye moyo
wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. [Isaya
26:3]
Kwa maana Bwana MUNGU,
Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu
zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. [Isaya
30:15B]
Na kazi ya haki itakuwa
amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. [Isaya
32:17]
bali wao wamngojeao Bwana
watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala
hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. [Isaya 40:31]
Amebarikiwa mtu yule
anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. [Yeremia 17:7]
Maana nayajua mawazo
ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa
ninyi tumaini siku zenu za mwisho. [Yeremia 29:11]
Bwana ni mwema kwa hao
wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na
kumngojea kwa utulivu. [Maombolezo 3:25, 26]
Njoni kwangu, ninyi nyote
msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu,
mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata
raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. [Mathayo
11:28-30]
Na amani ya Mungu, ipitayo
akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. [Wafilipi
4:7]
Kwa sababu hiyo nimepatikana
na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na
kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku
ile. [2
Timotheo 1:12B]
huku mkimtwika yeye fadhaa
zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. [1
Petro 5:7]
FURAHA
Nao wote wanaokukimbilia
watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi,
Walipendao jina lako watakufurahia. [Zaburi 5:11]
Utanijulisha njia ya uzima;
Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya
milele. [Zaburi 16:11]
Maana ghadhabu zake ni za
kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku,
Lakini asubuhi huwa furaha. [Zaburi 30:5]
Wapandao kwa machozi Watavuna
kwa kelele za furaha. [Zaburi 126:5]
Heri kila mtu amchaye Bwana,
Aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na
kwako kwema. [Zaburi 128:1, 2]
Na hao waliokombolewa na
Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya
vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia. [Isaya
35:10]
Hayo nimewaambia, ili furaha
yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. [Yohana 15:11]
Maana ufalme wa Mungu si kula
wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. [Warumi
14:17]