Mwalimu: Octavian Kinvyiro
Somo: KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU SIRI NI ROHO MTAKATIFU
Roho mtakatifu
ni Mungu, na Mungu ni neno. Nisingependa kuingia ndani zaidi kueleza Roho Mtatifu ni nani, majina
yake n.k Lakini kwa kifupi Biblia
inasema Roho mtakatifu ni Mwalimu, msaidizi ,mfariji na majina mengine mengi.
Kwa maana hiyo Roho Mtakatifu anauwezo wa kutuonesha kusudi la Mungu kwetu na anatufundisha
namna ya kuenenda katika kutimiza kusudi hilo na kutushauri. Mungu ni yeye Yule
jana, leo na hata Milele, alichofanya kwa manabii na Mitume hajaacha na wala
hataacha kufanya. Anafanya na zaidi kwa njia ya Roho Mtakatifu, tena sisi wa
agano jipya ndio zaidi kabisa, Yohane 14: 12, 16: 13,
Je,watu waweza kuongozwa na Roho Mtakatifu
ili kujua kusudi la Mungu?
Tulisema ili kuweza kujua kusudu la Mungu, kuna vitu tunaweza kuvitazama au kanuni ambazo tunaweza kuzifuata kama tulivyo ona hapo Mwanzo wa somo.Na kanuni hizo tulizoziona kwanza zaweza kutumika na watu au mtu yoyote atayeamua kukaa na kujichunguza ili kujua nini cha kufanya hapa dunia, bila kujua anatimiza kusudi la Mungu au la!, Kuna watu wametambua vipaji vyao na wanavitumia vyema kabisa. Kwamba wamempa Yesu maisha au la ni kitu kingine, lakini jambo ninaloamini ni kuwa shetani hana uwezo wa kumpa mtu kipaji, zaidi sana anatumia vipaji hivyo hivyo tulivyojaliwa na Mungu kujinufaisha yeye. Kwa hiyo mtu aweza akafuata ndoto zake, anajichunguza anaweza kufanya nini, akafuata msukumo wa ndani na akatimiza lile ambalo ni kusudi la Mungu, hata kama yeye mwenyewe hajui kama hicho ndicho alizaliwa kufanya kwa hapa dunia ili kutimiza fundisho la Katekismu ya kwamba tuliumbwa ili tumpende, tumtumikie na mwisho turudi kwake mbinguni, shetani haumbi, kila mtu aliumbwa na Mungu. Tumpendeje Mungu? Kwa moyo wetu wote, kwa akili zetu zote na nguvu zetu zote.
Kwa maneno
mengine kanuni ya Kufundishwa, kuelekeza na kushauriwa na Roho Mtakatifu ili
kujua na kutimiza kusudi la Mungu si kwa wote, bali ni kwa wakristu tu na si
wote pia bali wale waliokubali kuongozwa, kufundishwa na kushauriwa na Roho
Mtakatifu, kwani katika kutekeleza haya lazima Ushirikiano uwepo kati ya
Mfundishaji na mfundishwaji; mshauri na mshauriwa; mwongozaji na mwongozwaji. (This is two way traffic). Yachunguze
maandiko haya kupata nini nichomaanisha:
·
Yohane 3:1-12; 14:15-18; 25- 27;
17:15-22
Kanuni ya
Kuongozwa na Roho Mtakatifu ni Yetu wapendwa, Tumtumie na tumuulize,
tumsikilize. Ngoja nikupe mifano michache toka kwenye biblia ya namna
anavyosema na sisi katika kujua kusudi lake kwetu. Kumbuka biblia inasema Mungu
ni yeye yule jana, leo na hata milele, AMINA!
·
Isaya 30: 20- 21; Chunguza neno hilo kama waberoya (Mdo 17: 10-11).
Isaya 30: 20- 21; Chunguza neno hilo kama waberoya (Mdo 17: 10-11).
Naomba nikupe home work; Tazama kwa
makini maneno yafuatayo;
i.
Walimu wako hawatafichwa tena,
ii.
Ila macho yako yatawaona waalimu
wako,
iii.
Na masikio yako yatasikia neno nyuma
likisema, Njia hii ifuate,mgeukapo Kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo Kwenda
mkono wa kushoto.
·
Yoel 2: 28; Hata baada ya hayo , ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote
wenye mwili na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri; wazee wenu wataota ndoto,
na vijana wenu wataona MAONO; sina haja ya
kuelezea au kufafanua zaidi, naomba Roho Mtakatifu akufunulie upate ufunuo (revelation) wa binasfi juu ya neno hili; Ona, hajasema Baada ya kuwamiminia Roho Mtakatifu
wataanza kunena kwa lugha, nakulia
nakupiga kelele; hapana! Soma mwenyewe, na tafuta maana ya neno MAONO au VISION
kwa lugha ya Kiingerea.Yaani Wakristu hasa vijana tukimruhusu Roho Mtakatifu
atuongoze tutaweza kufanya mambo makubwa yanayooneka (tangible), na kubadilisha
ulimwengu huu.
·
1 Nyakati 29: 11-12
·
Mithali 16: 1-3
Haya ni
maandiko machache sana, kututhibitishia kuwa Tukikaa sawasawa na Roho
Mtakatifu; sky is the limit’ mafanikio ni lazima. Tungeweza kuona mifano
mingi ya watu walioshinda kwa kusikiliza na kutii sauti ya Roho mtakatifu twaweza
kukesha; Mungu hajabadilika. Mungu wa Ibrahim ndio Mungu wetu, Mungu ya Isaka
na Yakobo ndio Mungu wetu, Mungu Petro na Paulo jamani ndio huyo huyo, Mungu wa
Papa Yohane wa pili ndio huyo huyo Mungu wetu.
Tutaendelea
siku nyingine kujifunza na kuona vitu
au mambo gani ya kufanya au kutofanya
ili kutoa nafasi kwa Roho Mtakatifu kusema na sisi kwa Habari ya kusudi la
Mungu.