Papa awaasa Maaskofu kukemea anasa na utamaduni wa taka, kujilimbikizia mali na Ubinafsi.
Baba Mtakatifu akiwa na Maaskofu wenzake Philadelphia |
Jumapili Baba
Mtakatifu Francisko alikutana na Maaskofu wote waliokuwa wakihudhuria Mkutano
wa Nane wa Dunia wa Familia huko Philadelphia Marekani .
Hotuba ya Papa kwa
Maaskofu hao,ilionyesha furaha yake ya kuwa pamoja nao katika muda huo wa
kushirikishana tafakari za Kichungaji kwa maisha ya familia, chimbuko la
binadamu. Na pia iliwaasa Maaskofu kuwa macho na ongezeko la utamaduni wa taka,
unaorarua familia na jamii leo hii.
Papa alikumbusha
kwamba leo hii, tuko katika dunia ya ulaji na utupaji , tabia na mapenzi ya
kujilimbikizia mali, inayo chukuliwa kama ndilo jambo muhimu la mtu kujivunia.
Ubinafsi usiojali wengine, wala kuona umuhimu wa kujali hali za binadamu
wengine. Kama matokeo yakePapa anasema, , jamii zimegeuzwa
kuwa uwanja wa maonyesho ya ufahari wa tamaduni mbalimbali,
ulifungamanishwa na maonjo ya kulimbikiza mali na utupaji wa onvyo,
wakati familia zingine zikiwa hazina chochote cha kujikimu katika
mahitaji msingi.
Papa aliendelea
kuzitazama hali halisi za sasa , jinsi ambavyo kuna mabadiliko katika maduka na
masoko. Aliangalishwa kwa jinsi leo hii kunatengenezwa maeneo makubwa ya maduka
yanayoitwa “supermarket”, yaliyojazwa vitu kupindukia, akisema dunia hii
sasa inaweza kuitwa dunia ya utamaduni wa supermarket, wenye kuleta ushindani
mkubwa katika uzalishaji wa mali na ushindani zaidi wa nani ana vitu
vingi vipya kuliko mwingine. Hali iliyoua moyo wa mshikamano na umoja na
wengine, na kuvunja uaminifu katika mahusiano ya kijamii. Urafiki leo unajengwa
zaidi katika misingi ya utajiri. Wenye navyo wanawatafuta wenzao walio navyo.
Hivyo mambo yanayowaunganisha watu yanahusishwa zaidi na vitu alivyo navyo mtu.
Ile misingi ya kujaliana kama binadamu au jirani haipo tena, Ujirani
unajengwa zaidi katika misingi ya anasa na ulafi.
Papa ameonya,
matokeo yake ni kuwa na utamaduni wa taka, utamaduni wa kuchoka haraka na
vitu na kuvitupa , hata kama bado vinaonekana kufaa kutumia vinatupwa kwa
nia za kuwahi kununua mitindo mipya inayojitokeza katika masoko. Huu ni
uharibifu mkubwa , kwa kuwa kiundani hujenga moyo wa kubaguana. Wale wasioweza
kwenda na kasi hii ya utamaduni wa utupaji , hupata hisia za kuwa wanyonge na
wapweke. Upweke wenye kuwa na woga katika juhudi za kutimiza wajibu wao,
kwa kuwa hujiona hawezi kufanya lolote katika jamii maana hawana kitu.
Baba Mtakatifu
aliendelea kuhoji iwapo lawama zitupiwe vijana wanaokua katika aina hii ya
jamii, au kuwalaumu kwa kuishi katika ulimwengu wa aina hii. Aidha Papa alihoji
iwapo wachungaji wa kiroho, wahimize vijana kurudi kaika maisha ya ujima, kwa
kuwa dunia sasa inasambaratika wala mwisho wake haujulikani utakuwaje? Papa
alitoa hisia zake kwamba, hadhani kama ni sahihi kurudia maisha ya ujima.
Lakini Maaskofu kama wachungaji wa kanisa ni lazima kufuata nyayo za
Mchungaji mwema, wanatakiwa kuandamana na watu na kuwainua na kutibu majeraha
ya nyakati. Kuzitazama hali halisi, kwa jicho makini, kwa ajili ya
kutenda inavyopaswa , kazi za kichungaji zenye kuleta uongofu. Dunia ya leo
inahitaji uongofu wa moyo . Na hivyo inakuwa ni muhimu kwa kanisa leo hii
kusonga mbele kwa ushupavu zaidi kuihubiri Injili kwa watu wote mahali popote
nakatika matukio yote, bila kusita sita wa kuhofia kitu. Ni kuihubiri furaha ya
Injili kwa watu wote bila ubaguzi.
Na hivyo aliwahimiza
Maaskofu kuonyesha kushikamana na familia katika misingi ya kiinjili. Ni muhmu
tena lazima kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya jamii kujaliana, kuanza
kufanya mabadiliko ndani ya familia. Kusadikisha watu kwamba, familia ni habari
njema kwa maisha ya dunia hii iliyomezwa na moyo wa ubinafsi na utamaduni
wa taka.
Alikumbusha
katika maisha ya Kanisa, familia hupewa kipaumbele cha kwanza kwa
sababu, familia ni mpango wa Mungu katika maajabu yake ya uumbaji. Na
siku zote na mahali pote duniani, Kanisa linapaswa kuifurahia zawadi hii
ya Bwana kwa uwepo wa familia, hata wakati wa majaribu na matatizo ,
hubaki aminifu katika ahadi yake na katika kuitunza imani.
Baba Mtakatifu
aliendelea kuwaasa Maaskofu wenzake juu ya changamoto za Kichungaji zinazowakabili
leo hii katika nyakati hizi za mabadiliko makubwa. Hivyo akasisitiza Kanisa
kuwa na maamuzi thabiti katika kutambua zawadi hii kuu kutoka kwa Mungu. Papa
alirudia kusema, familia ni misingi wa agano kati ya Kanisa na uumbaji wa Mungu
. Bila familia , ina maana hata kanisa lisingekuwepo. Na hivyo Kanisa
lisingeweza kuwa ishara na chombo kinachounganisha binadamu na Mungu na umoja
wa kabila zote za binadamu.
Papa aliendelea
kuwataka Maaskofu wenzake kama wachungaji , kukusanya nguvu zao na kujenga
upya shauku kwa ajili ya kuendeleza familia katika mahusiano yake ya milele,
katika misingi ya utimilifu wa baraka za Mungu . Na kwamba, wanahitaji kuwekeza
nguvu zao zote , si katika tu kufanya rejea kwenye matatizo ya kidunia
yanayowazunguka , lakini katika uhalali wa uwepo wa familia ya Kikristo, kwa
kutoa mwaliko wa dhati na ujasiri kwa vijana ,ili wachague maisha ya ndoa
na familia.
Makala hii kwa mujibu wa radio vatican