KIPINDI CHA KWANZA.
Mwalimu: OCTAVIAN KIYVIRO SOMO: NAMNA YA KUTAMBUA KUSUDU MUNGU
Kichwa cha
habari hapo juu ni mwendelezo wa somo juu ya KUSUDI LA MUNGU katika maisha yetu. Somo lilotangulia
tuliyachunguza maandiko (mdo 17:10 - 12)
juu ya Kusudi la Mungu kwa kila mmoja.Tuliona mifano mbali mbali ya sababu ya
watu Fulani katika biblia ambao kwa uhakika kabisa walijua au walitambulishwa nini
kilichowaleta hapa dunia. Mungu hajabadilika ni yeye Yule jana leo na hata milele.Tuliumbwa kuja kujenga
ufalme wa Mungu hapa dunia.
Kila mmoja
ameumbwa kuja kutimiza assignment au jukumu Fulani. Na hili jukumu ni yeye tu atakaye litimiza si vyinginevyo. Ni vyema ikaeleweka kuwa kusudi la Mungu
tunalozungumza si kufanya vitu Fulani vya kiroho kama tulivyozoea kwa mfano
kuhubiri, kuwa padre au mwijilisti Fulani, ni zaidi ya hapo,Yawezekana mtu akawa
ni mkimbiaji, au mchekeshaji, akawa
anatimiza kusudi la Mungu anaweza kuwa mfanyabishara, kuwa mwanasiasa au
kufanya kazi Fulani akawa anatimiza kusudi la Mungu. Kwa neno la Mungu linasema panatofauti ya
karama lakini roho ni yeye Yule Yule. Pana tofauti za huduma lakini bwana ni
yeye Yule Yule anayehudumiwa.
Kwa mantiki hiyo ni vyema kijana kabla ya
kuwaza kuoa au kolewa akatafuta kwanza nini nilipi kusudi (assignment) la Mungu
katika maisha yake. Bila shaka tuliona kwa ufupi katika somo lililopita kuwa jukumu au kusudi
linatangulia ndoa. NDOA SI KUSUDI LAMUNGU BALI NI MPANGO WA MUNGU (Marriage is
not a purpose of God, but it is a plan of God). Kipi kinatangulia lengo au
mpango mkakati wa kutimiza lengo?
Nitakuonyesha
njia ambazo Roho mtakatifu amependa kutufundisha kwa namna ya tofauti
kabisa,Njia hizo kwa kweli ni practical yaan ni halisia, kama ukizifuata lazima
tukutane na assignment yetu toka kwa Mungu. Hakuna short cut/njia ya mkato
fuata njia au kanuni lazima ufanikiwe.
- Kwanza Mawazo au ndoto zetu za utoto.
Mara nyingi
katika umri Fulani hasa kuanzia miaka 8 hadi 12, mtoto anakuwa na mawazo ya
kutaka kuwa mtu Fulani au kufanya kitu Fulani.Haya mawazo ni vyema kuyafanyia
kazi. Sasa kwa sababu kwa namna moja au nyingine wazazi wengi hawatilii maanani
mawazo ya watoto wao katika kipindi hicho,yamkini vijana wengi wanafanya vitu
kinyume kabisa na mawazo waliyo kuwa nayo utotoni. Ni vyema ukachunguza mawazo
au vitu ulivyotamani kuvifanya ulipo kuwa katika umri huo. Yaweza kuwa hili
lilikuwa ni kusudi la Mungu.
Yesu akiwa
na umri wa miaka 12 anajua yeye ni mwalimu anawatoroka wazazi wake anaenda kwenye sinagogi na waalimu kwa maana nyingine wenzake,Tayari anajua nini
anachopaswa kufanya au ndoto hizo.
Tusome injili
ya luka 2:40-50; Yule mtoto akakua,akaongezeka nguvu,amejaa hekima,na neema ya
Mungu ilikuwa juu yake. Basi Wazee wake huenda
Yerusalemu kila mwaka,wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipokuwa na umri
wa miaka kumi na miwili,walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu;na
walipokwisha kuzitimiza siku,wakati wa kurudi
kwao,Yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake
walikuwa hawana habari.Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda
mwendo wakutwa,wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao. Na
walipomkosa,wakarejea Yerusalemu hukuwakimtafuta.Ikawa baada ya siku tatu
wakamwona hekaluni,ameketi katikati ya waalimu,akiwasikiliza na kuwauliza
maswali.Nao wote waliomsikiliza walistaajabu fahamu zake na majibu yake Na
walipo mwona walishangaa, na mama yake akamwambia, mwanangu ,mbona umetutenda
hivi? Tazama,babayako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.AKAWAAMBIA,kwani
kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?Nao
hawakuelewa na neno hilo alilowaambia.
Kumbuka Yesu
alikuwa ni mtu kweli kweli,kwa hiyo
yanayofanyika katika somo hapo juu,hakuna Mungu –Yesu ,ni Yesu Mtoto wa miaka
12 mwana Yosefu na Maria. Naomba uyachunguze maandiko uone jinsi ambavyo katika
umri huo anajua, anamawazo ya kuwa mwalimu, yupo hekulani anasikiliza na kuuliza
maswali kwa waalimu kwa sababu wazazi hawaelekei kuelewa mawazo yake,na ndio
maana kuwajibu hawakujua kwamba anapaswa kujifunza ualimu ili kutimiza ndoto
zake za kuwa mwalimu walaa hawakuelewa,kama wazazi wengine. Kuna mambo mengine ya kujifunza kupitia somo
(Injilii hapo juu).Lakini kwa ufupi chunguza mawazo aliyokuwa nayo kipindi
hicho yanakupa mwanga kujua kusudu la Mungu katika Maisha yetu
- Tazama au chunguza unawezakufanya nini,kwa maana talanta au kipaji chako
Kila mmoja
Mungu amemuumba tofauti na akampa talanta au zawadi au vipaji mbali
mbali.Katika kutambua na kuvitumia vipaji tulivyojaliwa na Mwenyezi Mungu,
twaweza kujua kusudi la Mungu katika Maisha yetu. Somo Injili ya mathayo
25:14
- Chunguza msukumo wa ndani (passion)
Yaani kuna vitu au kitu au kazi Fulani unatamani kufanya, na msukumo
ni mkubwa kabisa toka ndani. Wakati
mwingine unasukumwa bila kujua sababu.
Waweza kuona mtu Fulani anafanya kitu hicho yaani ndani mwako moto
unawaka,utamani ingekuwa wewe,waweza kufanya
kama ni kazi hata kwa bure au kwa malipo kidogo kwa jinsi unavyoipenda
- Siri ni Roho Mtakatifu
Kwa kweli
Roho mtakatifu ndo kila Kitu. Wakristu wengi tunafikiri Roho Mtakatifu ni kwa
ajili ya kunena kwa Lugha na mambo mengine kama hayo. Lakini kwa kweli Roho
Mtakatifu ni Mwalimu,Kiongozi, Mshauri. Si jambo la ajabu Roho Mtakatifu kutupa
wazo la kufanya Biashara Fulani au Kazi Fulani tena ya kuajiliwa au hata mambo ya siasa na katika hilo tukawa
tunatimiza kusudi la Mungu. Naomba nikupe mistari michache tu na bila shaka tutapata fursa ya kuingia
ndani zaidi katika eneo hili siku tukipata kibali,kwani sehemu hii ndo msingi wa
kila kitu katika kutambua kusudi la Mungu.
Zaburi 32;8. 1Mambo ya Nyakati
29:10-14,16-20, Yohani 16:13-15;Mathayo 21:10.
Roho Mtakatifu ni nafsi hai
kabisa,anasema,anahisi anaona wivu,n.k.
Tutaingia ndani zaidi kipindi
kitakachofuata,ili tujue siri za roho mtakatifu katika maeneo Mengi. Tumshukuru
sana Roho Mtakatifu kwa mafunuo yake na mengine mengi mbele yetu. Yohane
16:13-15
========================================================================
========================================================================
KIPINDI CHA PILI.
Mwalimu: AROBOGAST KANUTI
Mungu aliwapa Daniel na Yusuph,uwezo wa kupambanua mambo na
kupata majibu(solutions) ya vitu.
Tutambue Mungu amechoka theory, Mungu anataka aonekane
kwenye maisha yetu,tatizo sisi bado hatujawa tayari (serious), Mungu yeye yupo
tayari tangu zamani si sisi tu.
Paulo anamuhisia mtoto wake Timotheo 1timotheo 4:12-16 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe
kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo na katika Upendo na imani na
Usafi, hata nitakapokuja ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha, Usiache
kuitumia karama ile iliyomo ndani yako uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa
mikono na wazee, Uyatafakari hayo ukae
katika hayo ili kuendelea kwako kuwe dhairi kwa watu wote, Jitunze nafsi
yako na mafundisho yako, Dumu katika mambo hayo maana kwa kufanya hivyo
utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.
Yoshua
1:1-3, 5-8 “ Ikawa baada ya kufa kwake, Musa mtumishi wa
Bwana akamwambia Yoshua mwana wa Nuni,
mtumishi wa Musa akasema, Musa mtumishi wangu amekufa,haya basi ondoka, vuka
mto huu wa Yordani hata nchi niwapayo wana wa Israeli,Kila mahali
zitakapokanyaga nyao za miguu yenu nimewapa ninyi kama nilivyomwapia Musa tangu Jangwa hili na mlima huu lebanoni mpaka mto ule mkubwa,
mto Frati, nchi yote ya wahiti tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya
jua hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.
Tamani neno la Mungu liwe kweli, tuache hadithi “Yoshua 1:8 “Kitabu hiki cha torati
Kisiondoke kinywani mwako, bali yatafaki maneno yake mchana na usiku, upate
kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo, maana ndipo
utakapoifanikisha njia yako,kisha ndipo utakapositawi sana”
- Mtu asiudharau ujana wako
Usikubali mtu akaudharau ujana wako tukisoma kitabu cha
Walawi na Wafalme tunaona Mungu aliwaita vijana wadogo wa miaka 8,12 na
wakaweza kuwa wafalme katika nchi.Tutambue shetani yuko busy Kuvunja hiki
kizazi cha vijana wadogo na anajua mbele yako kuna mafanikio(your future is
Bright) na amekuwa akiwavunja hata vijana waliookoka.
Kanisa linategemea vijana na nchi inategemea vijana na
sisi ndio wa kuleta mabadiliko.
1Samweli 17:32-40, 41-46 “Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu
yeyote kwa ajili ya huyu, mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na mfilisti
huyu,Sauli akamwambia Daudi huwezi wewe kumwendea mfilisti huyu upigane naye,
maana wewe u kijana tu,na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake,Daudi akamwambia
Sauli, mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokua akija
simba au dubu, akamkamata mwana kondoo wa lile kundi mimi hutoka nikamfuata
nikampiga,nikamwua, Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia na huyu mfilisti
asiyetairiwa atakuwa mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye
hai, Daudi akasema Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba na makucha ya Dubu,
ataniokoa na mkono ya mfilisti huyu , Sauli akamwambia Daudi enenda na Bwana
atakuwa pamoja nawe”.
Mkaribishe Roho mtakatifu Katika masomo na mitihani yako na
Mtu awaye yote asiudharau ujana wako.
- Tupo ndani ya dunia hii, lakini sisi si wa dunia hii
Tutambue Roho Mtakatifu ni kila kitu na atatupasha mambo ya
baadae, maana aliwaonyesha akina Yusuph mambo ya miaka saba ijayo.Tukumbuke
Daudi alidharauliwa na Sauli, akadharauliwa na Eliabu kaka yake na Mfilisti pia
kwa kuonekana ni kijana mdogo.Roho mtakatifu yupo tayari kutuonyesha mambo
makubwa,Kile unachoongea wewe ndicho Mungu atakachotembea nacho, tusidharau
neno la Mungu maana halitastawi ndani yetu.Tunatakiwa kuwa mfano na kielelezo
siku zote na ufahamu wewe ni chumvi ya ulimwengu. Tito
2:6-8 “Vivyo hivo na vijana waume uwaonye
kuwa na kiasi, katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha
matendo mema na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, na
maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga
atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu”.
Uwe mfano Waefeso 4:29“Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani
mwenu, bali lililojema la kumfaa mwenye kuhitaji ili liwape neema wanaosikia”
Mungu anataka kukutumia kwenye viwango vya juu, tusitoe maneno maovu bali tuwe
faraja kwa wenzetu na wenye shida, Uwe mfano.
Maisha yako kuanzia unapoamka asubuhi mpaka jioni yawe
kielelezo na mfano katika mwenendo. Tito
2:8
Lazima uchague kuwa tofauti, usikubali kuenenda na ulimwengu
unakoenda,kama kijana, kubali kuwa tofauti ili kuleta mabadiliko.1Petro
4:3-4” Maana wakati wa maisha yenu
uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya mataifa kuenenda katika ufisadi na tamaa
na ulevi,na karamu za ulafi na vileo na ibada ya sanamu isiyo halali, mambo
ambayo wao huona ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi
ule ule usiokuwa na kiasi, wakiwatukana”.