CCCF HUDUMA YA KILA JUMATANO

Kuhusu CCCF na Huduma ya Vijana

CCCF ni mojawapo ya vikundi vya Sala vya Karismatiki Katoliki ndani ya Jimbo kuu la Dar es Salaam.Kikundi hiki kilianzishwa hapo mwaka wa 2009, na kinaendesha huduma zake chini ya ulezi wa Parokia ya Mt. Joseph na ni mahususi kwa ajili ya waamini wanaofanyakazi ama Biashara katika eneo la katikati ya Jiji. Lengo kuu la CCCF ni kupeleka injili kwa kundi hili kwa njia ya mahubiri,mafunzo,semina,kusifu na Kuabudu na Mengineyo.

CCCF ina Malengo makuu manne:
  • Kuimarisha Imani kwa waamini wote
  •  Kujenga umoja wa kanisa la Kristu
  •  Kupanua wigo wa Injili ili kuyafikia makundi mbalimbali yenye mahitaji tofauti,tofauti kwa mfano wa rika mbalimbali, watoto wenye mahitaji maalumu nk.
  •  Kubuni njia za kisasa za uenezaji wa Injili.

Majukumu ya CCCF:

Jukumu Kubwa la CCCF ni kuwainjilisha watu wa aina zote bila kujali dhehebu, dini,rangi,kabila na hata vyeo kwa sababu Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote.Hii ni katika kutii agizo la Bwana wetu Yesu Kristo ya kwamba, “Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi,na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahali”(mathayo 28:19-20