KIPINDI CHA KWANZA.
Mwalimu: OCTAVIAN KIYVIRO
SOMO: KUTAMBUA KUSUDI
LA MUNGU/ KUJUA KUSUDI LA MUNGU.
Matendo 17:11-12”Watu
hawa walikuwa waungwana kuliko wale wathesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno
kwa uelekevu wa Moyo,wakayachunguza maandiko kila siku,waone kwamba mambo hayo
ndivyo yalivyo.Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa kiyunani
wenye cheo, na wanaume si wachache”.
- Tuchunguze maandiko ili tuweze kujua Mungu
anazungumza nini kuhusu, Urafiki,Uchumba na ndoa.
Mithali
25:2”Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo,Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza
jambo”
- Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo ili sisi tuchunguze.
- Inatupasa Kutambua na kujua kusudi la Mungu.
- Kuna kusudi au sababu ya Mungu katika sehemu
uliyozaliwa.
Mathayo 1:18-21”Kuzaliwa kwake Yesu
Kristo kulikua hivi.Mariam mama yake alipokua ameposwa na Yusufu,kabla
hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho mtakatifu.Naye Yusufu
mumewe kwa vile alikua mtu wa haki,asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa
siri.Basi alipokuwa akifikiri hayo,tazama malaika wa Bwana alimtokea katika
ndoto, akisema, Yusufu mwana wa daudi usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana
mimba yake ni kwa uwezo wa Roho mtakatifu.Naye atamzaa mwan, nawe utamwita jina lake Yesu,maana, yeye ndie
atakae waokoa watu wake na dhambi zao”.
- Kuna sababu za
Mungu kukufanya uwepo duniani.
- Inatupasa kutafuta kusudi la Mungu.
Yeremia 1:4-5”Neno la Bwana
lilinijia, kusema kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua,na kabla hujatoka
tumboni nalikutakasa,nimekuweka kuwa nabii wa mataifa”
- Tutambue Kusudi la Mungu kwanza kwenye Maisha
yetu.
Hekima ya sulemani 7:3-6
- Yosefu alitambua kusudi la Mungu
- Tutambue Muunganiko wa neno la Mungu na
mahusiano.
Waamuzi
13:1-5”Malaika wa Bwana akamtokea Yule mwanamke akamwambia tazama wewe sasa
u tasa huzai,lakini utachukua mimba, nawe utazaa mtoto mwanamume.Basi sasa
jihadhari ‘nakuomba usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi,
kwani tazama utachukua mimba nawe utamzaa mtoto mwanamume, na wembe usipite juu
ya kichwa chake,maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni naye
ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya wafilisti”